Falsafa Yanga zinakwenda kubadilika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2020
Falsafa Yanga zinakwenda kubadilika

Ujio wa Kocha Cedric Kaze umepokelewa kwa furaha na mashabiki wa klabu ya Yanga kutokana na sababu kuu mbili

Kwanza Wanayanga wanafahamu asili ya soka la klabu yao, ni kushambulia na kufunga mabao

Kwa takribani misimu mitatu, utamaduni huo ni kama ulipotea tangu alipoondoka Mdachi Hans van Pluijm mwaka 2016

Babu Hans aliondoka na Yanga ile ya kukimbiza 'mpera-mpera'

Ni shauku la kila Mwanayanga kuona utamaduni ule unarejea, ujio wa Kaze umewapa matumaini mapya, kwa nini?

Kaze ni muumini wa soka la kushambulia, amelifundisha soka hilo hata kabla hajakwenda Ulaya mwaka 2012

Lakini pia, kafanya kazi kwenye Academy za FC Barcelona kwa takribani misimu mitano, ni wazi atakuwa ameiva kwelikweli kimbinu

Hakuna mtu asiyependa mifumo na kimbinu zinazotumiwa na Fc Barcelona, wanacheza 'tiki-taka', ni mwendo wa burudani na mabao tu

Pili, Wanayanga wanapenda kuona timu yao inarejesha ufalme wake katika soka la nchi hii na pengine sasa ni wakati wa kuvuka mipaka

Hii heshima ya kuitwa mabingwa wa kihistoria haikuja kwa bahati mbaya. Ukienda pale Jangwani yalipo Makao Makuu ya Yanga, ingia ofisi ya Mtendaji wa klabu ushuhudie utitiri wa Makombe

Changamoto za kiuchumi ziliiyumbisha timu misimu mitatu iliyopita ambayo watani zao Simba wametumia mwanya huo kujiimarisha

Lakini sasa baada ya GSM kufanya uwekezaji mkubwa hasa kwa usajili kabambe msimu huu, wengi wanadhani ni wakati wa Yanga kurejea mahali walipozoea

Kaze ameahidi kuwarejesha Yanga mahali hapo, na kuwa Wanayanga watarajie mambo makubwa kutoka kwake

Amesema ataboresha mbinu za timu akihakikisha wanatumia mfumo wa kisasa lengo likiwa kuwapa furaha mashabiki na wakati huohuo wakitimiza malengo yaliyowekwa

Kaze ametua Yanga huku akifahamu atakabiliwa na presha kubwa ya mashabiki ambao wamechoka kuumizwa na mwenendo wa timu yao

Ameonyesha utayari na kujivunia kujiunga na Yanga wakati huu, atafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha furaha ya Wanayanga inarejea

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’