Sasa ni rasmi kuwa kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze atatua kesho Alhamisi saa 5 usiku tayari kwa ajili ya kuanza kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria kuelekea mechi za ligi kuu pamoja na mashindano mengine.
Kaze anatua kuchukua nafasi ya Msebia, Zlatico Krmpotic ambaye alitupiwa virago mapema mwezi huu baada ya kudumu kwa siku 37 tu klabuni hapo.
Afisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kocha huyo raia wa Burundi atatua kesho usiku
"Ni rasmi kocha Cedric Kaze atatua kesho saa tano usiku tayari kwa kazi ya kuifundisha timu yetu kuhusu mkataba atakaosaini tutawaeleza baada ya kufika," amesema Nugaz.
Mapema leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Kaze aliweka wazi furaha yake kuelekea majukumu mapya katika klabu ya Yanga Yanga
ADVERTISE HERE