Kocha Mpya wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kujivunia kuwa kocha mkuu wa Yanga, moja ya klabu zenye historia ya kipekee barani Afrika
Kaze anayetarajiwa kuwasili nchini wakati wowote, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, ameeleza utayari wake kufanya kazi na mabingwa hao wa kihistoria Tanzania
"Najivunia kuwa kocha wa timu hii yenye historia kubwa, mashabiki wa kipekee na moja ya timu bora barani Afrika. Pamoja tutafanya makubwa," aliandika Kaze
Kocha huyo wa zamani wa Academy za Fc Barcelona, anasubiriwa kuanza majukumu yake ikielezwa anaweza kutua kesho Alhamisi
ADVERTISE HERE