Baada ya kusaini mkataba na Yanga, kiungo mshambuliaji Said Ntibazonkiza bado yupo nchini akizoea mazingira kabla ya kuanza majukumu yake ndani ya mabingwa hao wa kihistoria
Kulingana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Burundi ataanza kuitumikia Yanga Novemba 15, mwezi mmoja kabla ya kufunguliwa dirisha dogo la usajili
Mwamba huyu ataanza rasmi majukumu yake pale usajili wake utakapokuwa umeidhinishwa na TFF
Katika kipindi ambacho atakuwa anasubiri, fundi huyo ataendelea kujifua na wachezaji wengine ndani ya kikosi cha kocha Cedric Kaze ambaye inaelezwa usajili huu ni pendekezo lake
Ntibazonkiza kucheza namba 10, nafasi ya mshambuliaji msaidizi, kazi yake ikiwa kufunga na kuwatengenezea wengine nafasi
Huyu mwamba ni mchezaji aliyekamilika kwelikweli, Wanayanga wasubiri mambo mazuri kutoka kwake