Habari njema kwa Wanayanga ni kuwa wasiwe na presha kuhusu ujio wa kocha wao Cedric Kaze kwani pamoja na kuwa bado hajawasili nchini, alianza mikakati yake mapema tu
Kaze amefichua kuwa anaifuatilia Yanga tangu msimu huu ulipoanza. Ametizama mechi zote za ligi pamoja na zile za kirafiki
"Kwangu ni jambo muhimu kupata taarifa sahihi ya timu ili niweze kufahamu ukubwa wa majukumu yangu pale nitakapokuja Tanzania. Nimebahatika kutizama mechi zote ambazo Yanga wamecheza kwenye ligi na hata mechi za kirafiki," alisema Kaze
"Nimefuatilia kuanzia mchezo wa kwanza wa ligi ambao Yanga walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Prisons, nikaangalia mechi nyingine zote, lakini pia nimewafuatilia wapinzani wetu Simba, Azam Fc na Polisi Tanzania ambayo tutacheza nao mchezo unaofuata"
"Nimejiridhisha na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, wachezaji wa kigeni niliwafuatilia mapema hivyo nafahamu uwezo wao. Hata wachezaji wa hapo Tanzania kina Metacha, Feisal, Zawadi Mauya, Ditram Nchimbi, Bakari Nondo, Kibwana, Yassin na hata Farid Mussa aliyerejea kutoka Hispania, nimewafuatilia"
"Nafahamu mazingira ya viwanja hasa vya mikoani, nimefuatilia mechi za Yanga na hata wapinzani wetu kwa mechi walizocheza mikoani. Kikubwa nakuja nikiwa nafahamu kile napaswa kufanya ili nipate kufanikiwa," aliongeza Kaze
Wakati akitarajiwa kutua nchini wiki hii, Kaze tayari ametanguliza program zake za mazoezi zinazosimamiwa na kocha msaidizi Juma Mwambusi