Pamoja na Stars kupoteza mchezo wa kirafiki kwa kufungwa bao 1-0 na Burundi, Feisal Salum 'Fei Toto' ni mmoja wa wachezaji waliong'ara katika mchezo huo
Fei Toto alipewa jukumu la kuchezesha timu, akianza sambamba na Jonas Mkude na Said Khamis Ndemla
Kiungo huyo wa Yanga aliipendezesha Stars eneo la kiungo, pasi zake za uhakika, mara nyingi akiwa katika eneo analopaswa kuwepo
Fei Toto ni mchezaji anayeonyesha ukomavu wa hali ya juu msimu huu, ni suala la muda tu atatimiza ndoto yake ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi, hasa barani Ulaya
Ni mchezaji mwenye vigezo vya Kimataifa, muhimu kwake ni kuendeleza juhudi kuhakikisha anafikia malengo
Pamoja nae, nyota wengine wa Yanga waliopata nafasi kwenye mchezo huo ni beki kisiki Bakari Nondo Mwamnyeto na Ditram Nchimbi aliyeingia kwenye kipindi cha pili