Tanzania imepoteza mchezo muhimu wa kirafiki dhidi ya Burundi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Shuti la nje ya 18 lililopigwa na Saidi Ntibazonkiza kwenye dakika ya 85 lililotosha kuihakikishia Burundi ushindi huo muhimu ambao utawaongezea alama kwenye viwango vya FIFA
Stars ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini changamoto ilionekana kwenye umaliziaji
Iddi Selemani alikosa nafasi kadhaa za kuifungia Stars kama ilivyokuwa kwa washambuliaji wenza Saimon Msuva na Mbwana Samatta
Stars ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji pungufu baada ya Jonas Mkude kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano
Burundi ilitumia vyema idadi pungufu ya wachezaji wa Stars kwani iliuchukua mchezo moja kwa moja baada ya Mkude kutolewa
Etienne Ndayiragije Mkufunzi wa Stars bado ana kazi ya kurekebisha makosa hasa upande wa ushambuliaji kabla ya kwenda kule Tunisia Novemba 13