Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kukutana leo Jumatatu kujadili shauri lililowasilishwa na Yanga linalohoji uhalali wa mkataba wa Bernard Morrison na klabu ya Simba
Wiki iliyopita uongozi wa Yanga kupitia Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela ulipeleka malalamiko TFF wakidai mkataba aliosaini Morrison na klabu ya Simba ni batili kwani una mapungufu mengi
Ikumbukwe awali kamati hiyo ilimtangaza Morrison kuwa mchezaji huru baada ya kubaini mkataba aliokuwa amesaini na klabu ya Yanga kuwa na mapungufu
Hivyo uongozi wa Yanga umetaka uamuzi uliochukuliwa dhidi yao, uchukuliwe na kwa upande wa Simba kwani mapungufu waliyobaini yako sawasawa na mapungufu yaliyopelekea mkataba wake na Yanga ubatilishwe
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Elias Mwanjala amesema Kamati itakutana kujadili shauri hilo, taarifa itatolewa kwa uamuzi wowote utakaochukuliwa