Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kupimana ubavu na Burundi katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ambao uko katika kalenda ya FIFA
Mchezo huu ni maalum kwa kocha Etienne Ndayiragije kukipima kikosi chake kabla ya mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 21 dhidi ya Tunisia mwezi ujao
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri, ambapo Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
Ndayiragije anatarajiwa kutumia kikosi chake kilichokamilika ambacho kitaongozwa na nahodha Mbwana Samatta
Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa kuiunga mkono timu yao ya Taifa
Stars inatuunganisha Watanzania wote hivyo siku ya leo tuna jambo letu pale kwa Mkapa
ADVERTISE HERE