Huyu Carlinhos sio wa kucheza winga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2020
Huyu Carlinhos sio wa kucheza winga

Kwa dakika chache alizocheza nafasi ya kiungo namba nane akishiikiana na Mukoko Tomombe, fundi Carlinhos aliifanya Yanga itembee zaidi kuelekea lango la Mwadui Fc jana kwenye mchezo wa kirafiki ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Akiwa hana mambo mengi, Carlinhos ni hodari sana kwenye kupiga pasi. Huyu mwamba anagusa mpira mara mbili tu, anatuliza kisha anatoa pasi

Carlinhos ni mchezaji ambaye anaweza kupiga pasi fasaha akiwa umbali wa zaidi ya mita 30! Mguu wa huyu mtu sio wa kawaida

Kwa wastani ametengeneza nafasi ya bao katika kila mchezo ambao amecheza

Kumtumia pembeni nadhani kunaikosesha Yanga ubunifu wake hasa katika kuifanya timu ishambulie kwani ni mchezaji mwenye akili ya kuifanya timu ishambulie, pasi zake anapiga kuelekea langoni kwa adui

Aliyekuwa kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic hakuwa na mbinu nyingi, hivyo akimtumia pembeni kwa ajili ya kupiga krosi tu

Lakini Carlinhos ana vitu vingi zaidi ya kupiga krosi na faulo. Anaweza kuchezesha timu na pia anaweza kufunga pia

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’