Kabwili aongezwa Kilimanjaro Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
30 Nov 2017
Kabwili aongezwa Kilimanjaro Stars
Kocha Mkuu wa Tanzania Bara, ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje, ameongeza nyota watatu katika kikosi chake mara baada ya Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA), kuridhia kuongezwa wachezaji watatu kwa kila timu.

Awali, CECAFA ilihitaji wachezaji 20 tu, lakini sasa wameongeza watatu na kufanya idadi mpya ya wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ya Chalenji kwa mwaka huu kuwa 23.

Wachezaji walioongezwa na Kipa Ramadhani Kabwili kutoka Yanga, Amani Kiata wa Nakuru All Stars ya Kenya na Yahya Zayd kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.

Kikosi cha wachezaji 20 wa awali wa Ninje - Kocha wa Daraja ‘A’ la Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), ni makipa Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United).

Walinzi ni Gadiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Yanga), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).

Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Yanga).

Washambuliaji ni Mbaraka Yussuph (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman), Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).

Benchi la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3, mwaka huu, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na Libya ambayo ni timu mwalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika.

Kilimanjaro Stars ambayo imewahi kutwaa mara tatu taji hilo la Chalenji tangu kuanzishwa kwake, itaaza kampeni za kurudisha heshima yake dhidi ya Libya katika kundi hilo la A utaofanyika Desemba 3, mwaka huu.

Jumla ya timu shiriki kwenye CECAFA Senior Challenge Cup mwaka huu itakuwa 10 ambazo ni pamoja na wenyeji Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, South Sudan, Ethiopia, Zanzibar, Somalia, Libya na Zimbabwe iliyojitoa.

Sudan wenyewe wamejiondoa katika mashindano ya mwaka huu wakati mataifa mawili ya Eritrea na Djibouti nayo hayatashiriki.

Michuano hiyo itatumia viwanja vya Moi kilichopo Kisumu (Moi Stadium), Bukungu kilichopo Kakamega na Afraha kilichopo Nakuru wakati Uwanja wa Kasarani Nairobi na ule wa Kenyatta uliopo Machakos vitatumika kama viwanja vya ziada.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →