Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Oktoba 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabingwa hao wa kihistoria waliingia kambini mapema wakijua Oktoba 18 wanakwenda kuchuana na watani zao Simba lakini mchezo huo ukasogezwa mbele mpaka Novemba 07
Juma Mwambuzi ndiye Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga sasa wakati akisubiriwa Cedric Kaze anayekwenda kurithi mikoba iliyoachwa na Zlatko Krmpotic
Mwambusi alianza kusimamia mazoezi ya Yanga juzi ambapo amewaongezea wachezaji muda wa kufanya mazoezi ikilinganishwa na wakati wa Krmpotic, sasa wachezaji wanafanya mazoezi mara mbili kwa siku
Moja ya sababu zinazotajwa kumuondoa Krmpotic ni udhaifu wa program zake za mazoezi ambapo wachezaji hawakufanya mazoezi kwa muda mrefu
Aidha tayari Kaze anawasiliana na Mwambusi, bila shaka program za mazoezi wanayofanya wachezaji sasa, zinatolewa mtaalamu huyo raia wa Burundi
Yanga ina takribani siku 12 za kujiandaa kabla ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania