Kumekuwa na mjadala mkali kufuatia uamuzi wa Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 18 na kuusogeza mbele mpaka Novemba 07
Kwa mujibu wa ratiba ya CAF, mchezo huo pia unaweza usipigwe hiyo Novemba 07 kwani ratiba ya michuano ya kufuzu AFCON 2021 inaonyesha Novemba 13 Stars inapaswa kuwa nchini Tunisia kuumana na wenyeji wao katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2021

Bodi ya Ligi imetaja sababu ya kusogeza mchezo huo mbele ni kutokana na hofu ya wachezaji wa kigeni walioitwa timu za Taifa wanaweza kuchelewa kutokana na changamoto ya usafiri iliyosababishwa na corona
Hata hivyo ni klabu ya Simba inayoonekana kuwa na hofu ya kuwakosa wachezaji wake Luis Miquissone na Clatous Chama ambao wameitwa timu za Taifa za Msumbiji na Zambia
Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba waliotwa timu za Taifa ni Joash Onyango na Francis Kahata walioitwa Kenya