Mkuu wa idara ya Habari klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema mauzo ya tiketi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Oktoba 18 katika wa Taifa, zitaanza kuuzwa mapema
Bumbuli amesema wiki hii wanatarajiwa kufanya kikao na Serikali kuandaa utaratibu wa mauzo ya tiketi
"Tumepanga kukutana na wenzetu wa Serikali wiki hii ili kuandaa utaratibu wa mauzo ya tiketi. Lengo tuanze kuuza tiketi mapema, mashabiki wanunue ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo," alisema
Akizungumzia maandalizi ya kikosi, Bumbuli amesema timu tayari imeingia kambini kujiandaa na mchezo huo
"Mchezo huo hauna tofauti na michezo mingine, hivyo maandalizi yake hayana tofauti. Sisi tunaiandaa timu yetu kwa ajili mechi zote za ligi pamoja na michuano ya kombe la FA"
Baada ya mapumziko ya siku mbili, jana Yanga iliingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo huo
Β