Pluijm alichora mstari wa mafanikio

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
5 Oct 2020
Pluijm alichora mstari wa mafanikio

Misimu ya 2014/15 na 2015/16 inabaki kuwa misimu bora sana ya Yanga katika kipindi cha miaka 10 iliyopita

Ni wakati huo ambao Yanga ilikuwa haikamatiki, ikicheza kandanda la burudani lililoambatana na idadi kubwa ya mabao

Mdachi Hans van Pluijm ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa Mabingwa hao wa kihistoria akisaidiwa na Charles Mkwasa na baadae Juma Mwambusi, huyuhuyu kocha msaidizi wa Yanga sasa

Ni zama ambazo bado zinawaumiza Wanayanga kwani tangu wakati ule hawajashuhudia tena timu yao ikichezwa katika kiwango kile

Yanga inasaka kocha mwingine baada ya kumtimua Mserbia Zlatko Krmpotic aliyedumu kwa siku 37 tu

Amini, usiamini, Pluijm anaweza kuwa chaguo sahihi kurejea pale Yanga

Tofauti na makocha wengine wanaotajwa, Pluijm ndiye kocha wa mwisho kuifanya Yanga icheze vile wanavyotaka mashabiki

Uzoefu wake na soka la Tanzania inaweza kuwa faida zaidi kwake kulinganisha na makocha wengine

Wakati huu msimu ukiwa unaendelea, kumleta kocha ambaye hafahamu vyema soka la Tanzania kunaweza kuwa na athari

Kwa aina ya wachezaji ambao Yanga inao, kwa Pluijm inaweza kuwa kazi rahisi kuwaunganisha ndani ya muda mfupi

Kwani Pluijm ni kocha asiyehitaji muda mrefu kuifanya timu icheze kandanda la ushindani

Rejea alipoondoka Yanga na kujiunga na Singida United, baada ya muda mfupi tu akaifanya Singida United kuwa timu tishio

Pamoja na kuwa hakukaa Azam Fc kwa muda mrefu, aliweza kuifanya Azam kucheza soka la kuvutia

Wanayanga wametega sikio wakisubiri kumfahamu mrithi wa Krmpotic

Wakati huu wengi hawatapenda kuona uongozi unafanya bahati nasibu kama ilivyokuwa kwa kocha aliyepita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’