Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezitaka klabu kuajiri maofisa habari wenye sifa
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Wallace Karia alisema klabu zote zimeajiri wahamasishaji badala ya maofisa habari.
Karia alisema utaratibu wa kuajiri maofisa habari uliletwa na Fifa lakini klabu hazizingatii sheria kuhusu ajira za watumishi hao.
"Ofisa Habari anatakiwa kuwa mwandishi wa habari lakini utaratibu umebadilika sana, lengo halikuwa hilo," alisema Karia
Leo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajiwa kutoa mafunzo kwa wasemaji wa vilabu

ADVERTISE HERE