Krmpotic ameacha 'ukuta wa Berlin'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2020
Krmpotic ameacha 'ukuta wa Berlin'

Pamoja na ukosoaji katika mbinu zake, aliyekuwa kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic anaweza kupongezwa kwa kuimarisha nidhamu kwenye ulinzi

Kabla ya ushindi mnono dhidi ya Coastal Union jana, kikosi cha Krmpotic kilikuwa kikipata ushindi wa kudokoa lakini nidhamu kwenye eneo la ulinzi imeonekana

Yanga imeruhusu bao moja tu katika michezo mitano, pale ilipolazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa kwanza wa msimu huu

Mabingwa hao wa kihistoria hawajuruhusu bao katika mechi zilizofuata iwe kwenye ligi na hata mechi za kirafiki

Krmpotic ameondoka huku timu yake ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi

Ameshinda mechi nne, sare moja huku timu ikifunga mabao saba

Ukuta wa Metacha, Yassin, Kibwana, Lamine na Mwamnyeto wakishirikiana na viungo Feisal, Mukoko na Mauya, wamefanya kazi yao ipasavyo

Lakini pia mafanikio haya yamechagizwa na usajili makini uliofanywa na GSM katika kuboresha safu ya ulinzi

Ujio wa Mwamnyeto umeimarisha maradufu eneo la ulinzi wa kati akitengeneza pacha imara sana na Lamine Moro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’