Kuna watu walinza kuhoji uwezo Carlinhos huku watani wakichombeza kuwa ni mchezaji wa mipira ya kutengwa tu na kuwa hawezi kung'ara katika mechi zenye ushindani
Lakini jana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, Carlinhos amedhihirisha kuwa ni mchezaji aliyekamilika
Carlinhos alifunga bao katika mazingira ambayo yalihitaji uwezo binafsi kuweza kuiwahi krosi ya Kisinda
Alikuwa hatari kila mpira ulipokuwa mguuni mwake, uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi ndefu na krosi unamfanya kuwa mchezaji wa kipekee kwenye kikosi cha Yanga




Katika mechi nne alizocheza kwenye ligi, ametengeneza mabao mawili huku mwenyewe akifunga bao moja
Carlinhos anaonekana kuanza kuizoea ligi ya Tanzania, dalili za msimu bora zimeanza kuonekana kwake
ADVERTISE HERE