Yanga inapambana kulinda heshima na taswira yake baada ya kitendo kilichofanywa na klabu ya Simba kumsajili Bernard Morrison ambaye alikuwa na mkataba halali na mabingwa hao wa kihistoria
Simba walifanikiwa kuifanyia 'umafya' Yanga kwa kuwatumia 'watu' wake ambao wako ndani ya TFF
Jana uongozi wa Yanga ulitangaza kufungua upya malalamiko yake baada ya kubaini mkataba aliosaini Morrison na Simba una mapungufu zaidi ya yale yaliyotumika kubatilisha mkataba wake na Yanga
Yanga kurejesha kesi hiyo TFF inamaanisha wanataka watu walewale waliofanya maamuzi mwanzo wakae tena watoe maamuzi mapya jambo ambalo halionekani kutokea
Kwa jicho la kawaida unaona wazi uwezekano wa kesi hiyo kupinduliwa ni mdogo sana na pengine ni vyema Yanga ikaendelea kukomaa na shauri hilo kule FIFA na CAS
Habari njema ni kuwa mpaka sasa mfumo wa usajili wa FIFA 'TMS' unamtambua Morrison kuwa mchezaji halali wa Yanga hiyo ikimaanisha kuwa Simba wameshindwa kusajili mkataba wake kule
Jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alithibitisha kuwa Mkataba wa Morrison unatambulika katika usajili wa TFF tu na sio FIFA. Ukiingia kwenye mfumo wa FIFA unasoma Morrison ni mchezaji wa Yanga
Yanga inapaswa kuendelea kuipigania haki yake huko huko majuu kwani kwa sarakasi zilizotokea mwanzo, utakuwa muujiza kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kutoa maamuzi ya kuubatilisha mkataba wa Morrison na Simba, maamuzi ambayo yatapelekea Simba kunyang'anywa alama zote ambazo walizipata katika mechi zote walizomtumia Morrison