Baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union keshokutwa Jumamosi ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga haitashuka tena dimbani mpaka Oktoba 18 itakapowavaa watani zao Simba
Mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 11, sasa utachezwa Oktoba 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabadiliko haya yametokana na uwepo wa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Burundi ambao utapigwa Oktoba 11
ADVERTISE HERE