Huyu mwamba apewe heshima yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2020
Huyu mwamba apewe heshima yake

Ukiangalia takwimu, kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic hana baya pamoja na kuwa ndio kwanza mwezi mmoja umetimia tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria

Ushindi wa mabao 2-0 ambao Yanga iliupata dhidi ya KMKM jana katika mchezo wa kirafiki, unamfanya awe ameshinda mechi sita kati ya saba alizocheza (ligi na mechi za kirafiki)

Alishinda mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir, akalazimishwa sare mchezo dhidi ya Prisons kisha akashinda michezo ya Mbeya City, Mlandege, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na jana KMKM

Katika soka, kocha mzuri ni yule anayeisaidia timu kushinda, kwani kinachotakikana kwenye soka ni alama tatu tu

Haijalishi umechezaje lakini kama unashinda hilo sio tatizo

Pale Uingereza hakuna kocha ambaye mbinu zake zinakosolewa kama Jose Mourinho ambaye kwa sasa anaiona Tottenham

Lakini Morinho ametwaa mataji yote barani Ulaya katika ngazi ya vilabu, akiwazidi makocha wengi tu ambao wanasifika kwa timu zao kucheza soka la kuvutia

Kumekuwa na presha kubwa kwa Krmpotic, wasioitakia mema Yanga nao wamechukua nafasi kukoleza moto ili kuhakikisha kocha huyu anatimuliwa kabla ya mchezo dhidi ya Simba

Hili litakuwa jambo la kushangaza kama uongozi wa Yanga utaingia 'mkenge'. Unamfukuzaje kocha ambaye ameshinda zaidi ya asilimia 90 ya mechi alizocheza?

Wengi wetu hatuna utaalam wa ukocha lakini tunadhani tunafahamu zaidi kuliko waliosomea, tunashinikiza yale tunayoyataka sisi ndio yafanyike

Msimu huu Wanayanga hawapaswi kukubali kuyumbishwa, wanaoanzisha hii mijadala wana malengo yao

Wanajua kama Yanga itamtimua kocha leo, inaweza kupoteana kwa mechi kadhaa pale kocha mpya atakapokuwa akitengeneza kikosi chake. Hii ni nafasi kwao kutimiza malengo

Umoja uliionyeshwa kwa kuvikataa baadhi ya vyombo vya habari vinavyoonekana kutumika, basi umoja huohuo uonekane kuwakataa wale wanaoshinikiza Krmpotic aondoshwe kwani hawana nia nzuri na Yanga

Kocha anafukuzwa pale timu yake inapokuwa haifanyi vizuri, huu utabiri unaofanywa na baadhi ya watu kuwa chini ya kocha huyu Yanga haitafanya vizuri huko mbeleni sio sahihi

Wasioelewa ratiba ya Yanga ya ligi ilipangwa kimkakati zaidi ukilinganisha na watani zao Simba. Yanga imeanza na timu vigogo kama Tanzania Prisons, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, timu ambazo ni kawaidia kushinda mechi dhidi yao huwa sio jambo rahisi

Lakini Krmpotic ameivusha timu salama katika mechi hizo, pamoja na muda mfupi aliokaa na timu anastahili pongezi

Hakuna muujiza ambao utatokea kuifanya Yanga icheze kama wanavyotaka mashabiki, wachezaji wengi ni wageni, watahitaji muda kuelewana

Nafikiri presha ya mashabiki kwa sasa iwe katika kuhakikisha timu inashinda kila mchezo na sio jinsi timu inavyocheza kwani ukicheza vizuri bila ya kupata matokeo ni kazi bure

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’