Krmpotic kutumia mechi za kirafiki kusaka muunganiko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2020
Krmpotic kutumia mechi za kirafiki kusaka muunganiko

Licha ya kikosi chake kutoa 'dozi' katika mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Zlakto Krmpotic, amesema mkakati wake kwa sasa ni kupata michezo ya kirafiki zaidi, ili timu yake icheze kwa kuzoeana na kupata muunganiko bora na hatimaye kutimiza malengo

Yanga inatarajia kuwakaribisha KMKM ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini, Dar es Salaam.

Mserbia huyo amesema licha ya kushinda katika mechi zao tatu za ligi, wachezaji wake wameonyesha kupambana licha ya kutokuwa na muunganiko mzuri kwa sababu ya kukosa matayarisho ya kuanza kwa ligi hiyo.

Zlatko alisema licha ya kuhitaji muda na kutumia mechi za ligi kutafuta matokeo pamoja na kupata muunganiko, pia mechi za kirafiki wanazocheza zinasaidia wachezaji wake kupata uzoefu na muunganiko mzuri.

"Sasa hivi hatuna muda wa kupoteza, tunatumia mechi za ligi kutafuta matokeo chanya, lakini kujenga kombinesheni kwa wachezaji wangu, pia kutumia muda huu kupata mechi za kirafiki ambazo nazo zitanisaidia kupata kile ninachokitarajia ndani ya kikosi changu,” alisema Zlatko.

Alisema kulingana na mapungufu ambayo amekuwa akiyaona katika kikosi chake, kubwa ni suala la muunganiko jambo ambalo analifanyia kazi kwa kupata mechi za kirafiki pamoja na kwenye ligi hiyo.

"Suala la ushambuliaji nalo bado hii inatokana na timu hiyo kutopata muda wa kukaa pamoja, haijalishi tunashinda bao 1-0 kila mechi kikubwa ni kupambana kutafuta pointi tatu zitakazotuweka katika nafasi nzuri na kufikia malengo yetu," alisema Zlatko.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
47m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’