Lunyamila aitabiria ushindi Yanga mechi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Sep 2020
Lunyamila aitabiria ushindi Yanga mechi dhidi ya Simba

Baada ya kumaliza kibabe ratiba ya mechi mbili za mikoani, kabla ya kukutana na Simba Oktoba 18 Yanga itaendelea kubaki jijini Dar es salaam, ikicheza mechi nyingine mbili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Hii ni nafasi kwa mabingwa hao wa kihistoria kujiimarisha zaidi kabla ya kukutana na watani zao Simba ambao wanapaswa kwenda kucheza na JKT Tanzania(Dodoma) na Tanzania Prisons(Rukwa) kabla ya mchezo wa Oktoba 18

Winga wa zamani wa Yanga Edibily Lunyamila amesema ratiba hiyo inaweza kuwanufaisha Yanga kwani tofauti na watani zao, wao watakuwa na muda wa kucheza na kuuzoea uwanja wa Mkapa

"Yanga watakuwa na faida ya wachezaji kupata muda wa kupumzika na kuuzoea zaidi uwanja wa Mkapa. Mechi watakazocheza kwenye uwanja huo kabla ya kukutana na Simba naamini zitawafanya wawe kwenye kiwango bora"

"Mechi za mikoa zina changamoto kuanzia kwenye viwanja, ni wazi Yanga hawatakubali kupoteza mechi dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania baada ya kupata matokeo kule Kagera na Morogoro. Simba wao wanakwenda kucheza kwenye viwanja vigumu, na ikitokea hawakushinda mechi zao, inaweza kuathiri morali za wachezaji wao kuelekea mchezo dhidi ya Yanga," Lunyamila amenukuliwa na gezeti la Mwanaspoti

Yanga inachanga 'karata' zake kuhakikisha wanashinda mchezo huo dhidi ya watani zao Oktoba 18

Tayari wamerejea mazoezini kujiwinda na mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi lakini, kesho Jumatano watatest mitambo dhidi ya KMKM katika mchezo wa kirafiki

Kocha Zlatko Krmpotic bado anahitaji wachezaji wake wapate mechi nyingi ili kutengeneza muunganiko wa kikosi chake

Yanga inaweza kucheza mechi mbili za kirafiki kabla ya mchezo wa Oktoba 18

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’