Afisa Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa winga Farid Mussa haonekani kikosini kwa kuwa alipewa ruhusu maalum baada ya kuugua
Farid hakuwa sehemu ya kikosi kilichoivaa Mtibwa Sugar jana katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Pia alikosa mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar
"Farid alipewa ruhusu maalum baada ya kuugua Malaria, hata hivyo sasa anaendelea vizuri. Mashabiki msiwe na wasiwasi siku sio nyingi mtamuona kijana wenu uwanjani," alisema Nugaz
Farid na Mapinduzi Balama hawakujumuishwa kwenye msafara wa Yanga uliokuwa mkoani Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar jana
ADVERTISE HERE