Tulieni dozi zinakuja - Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Sep 2020
Tulieni dozi zinakuja - Mwambusi

Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema pamoja na benchi la ufundi kukaa na timu kwa takribani siku 20, mabadiliko ya kiuchezaji yameanza kuonekana

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Yanga wamesepa na alama zote tatu kwa ushindi wa bao 1-0, Mwambusi amesema leo waliingia kimbinu zaidi kutokana na kufahamu mazingira ya uwanja sio rafiki

Aidha Mwambusi amewataka mashabiki wasiwe na hofu kuhusu timu yao kwani wakati utafika wataanza kugawa dozi nene kwa wapinzani wao

"Kocha amekaa na timu siku 20, unaona kabisa timu inabadilika na inatengenezeka taratibu. Kuna muda tutaanza kutoa dozi goli 10 , 8 siku chache zijazo

"Kumtumia Carlinho pembeni ilikuwa mbinu ya mchezo, ni mchezaji mzuri ambaye mipira yake huwa na madhara kwa wapinzani, hivyo tulilazimika kumweka pembeni ili apate nafasi ya kucheza bila kuzongwa

"Mapungufu ya leo unaenda kuyafanyia kazi na tutarudi tukiwa bora zaidi mchezo ujao dhidi ya Coastal Union," amesema

Yanga imeshinda mechi zote mbili za ugenini, ukuta wao ukiondoka na 'cleansheet'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’