Alama nyingine tatu kibindoni mkoani Morogoro baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar. Mabingwa wa kihistoria Yanga wanaendelea kufukuza mwizi kimyakimya
Ulikuwa mchezo mgumu uliojaa matumizi ya nguvu huku mipira mingi ya juu ikitumika zaidi kutokana na mazingira ya uwanja wa Jamhuri
Combination ya Carlinhos na Lamine imelipa kwa mara ya pili kwani ulikuwa mpira wa kona wa Carlinhos uliojazwa kimiani na Moro


Kwa mazingira ya uwanja wa Jamhuri, mchezo leo haukuhitaji ufundi, muhimu kilichohitajika ni alama tatu ambazo zimepatikana
Ni rekodi ya ushindi wa asilimia 100 ugenini, sasa mabingwa hao wa kihistoria wanarejea jijini Dar es salaam uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Coastal Union Oktoba 04
Msako wa alama tatu unaendelea, kampeni hii ni kila mechi..!