Mohammed Rashidi asubiri mwito wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2017
Mohammed Rashidi asubiri mwito wa Yanga
Mshambuliaji wa Prisons Mohammed Rashidi amesema yuko tayari kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga kama uongozi wa pande zote mbili utafikia makubaliano.

Rashidi kinara wa upachikaji mabao katika timu hiyo sasa akiwa na mabao sita, amesema bado ana mkataba na Prisons hivyo hawezi kuondoka kama makubaliano hayajafikiwa.

Rashidi alikuwemo kwenye kikosi cha Prisons kilichotoka sare ya bao 1-1 na Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 11 Jumamosi iliyopita.

"Sina tatizo kujiunga na Yanga kama watafikia makubaliano na waajiri wangu wa sasa Prisons," alisema Rashidi.

"Mkataba wangu bado haujamalizika, utamalizika mwishoni mwa msimu hivyo kwa sasa mimi bado ni mchezaji halali wa Prisons."

Yanga inayokabiliwa na michuano ya klabu mwakani imedhamiria kusajili washambuliaji wawili mmoja akiwa wa Kimataifa na mmoja kutoka ndani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’