Kampuni ya La Liga ambao walipewa jukumu la kupendekeza mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga, mwanzoni mwa mwezi ujao wanatarajiwa kukabidhi ripoti ya mwisho ya mapendekezo yao kwa uongozi wa Yanga
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Hersi Said, amesema wiki ya mwanzo ya mwezi Oktoba watapokea ripoti hiyo kutoka Kampuni La Liga kupitia Klabu ya Sevilla.
Aidha, Hersi amesema mchakato umefika hatua nzuri na ripoti hiyo ni ya mwisho tayari kuelekea hatua inayofuata katika kukamilisha mchakato huo
Alisema baada ya hatua ya kwanza ya makabidhiano, watapata utaalamu wa ndani, na kisha watautoa nje kwa kushirikisha matawi yote ya Yanga nchini nzima.
"Baada ya kupata utaalamu huo katika matawi yote ya Yanga kuelimisha na kupata ushauri wa wanachama kutokana na ripoti hiyo baadaye itapelekewa katika mkutano mkuu kupata ridhaa ya wanachama wote.
"Niwaombe mashabiki na wanachama wa Yanga, kuunga mabadiliko hayo ya kimfumo kwa sababu baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo tutawashikirisha wanchama wetu kabla ya kupeleka katika mkutano mkuu," alisema Hersi.
Alisema pia mashabiki wajitokeze kwa wingi kusapoti timu yao ikiwa ni pamoja na kununua jezi halali na kujitokeza kwa wingi katika viwanja inapocheza timu yao.