Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wake wajitokeze kwa wingi siku ya Jumapili kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Jamhuri
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini ikitokea Kagera ambako ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema huu ni msimu wao hivyo wajitokeze kwa wingi kuipa hamasa timu kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
"Jumapili hii saa 10 kamili pale Uwanja wa Jamhuri Morogoro tuna shughuli yetu maalum dhidi ya Mtibwa Sugar hivyo basi wanachama, wapenzi na Mashabiki mjitokeze kuipa hamasa timu yetu," alisema Nugaz
"Tumefanya maandalizi mazuri, wachezaji wameahidi na watahakikisha wanawapa furaha mashabiki, tuje kwa wingi kuwangezea hamasa"
Yanga inatarajiwa kutua mkoani Morogoro leo kukamilisha maandalizi kuelekea mchezo huo