Baada ya kujifua kwa takribani siku tatu, Yanga itaondoka leo Alhamisi kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Jamhuri.
Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri tayari kuelekea mkoani Morogoro kutafuta alama tatu.
Nugaz amesema watapata siku mbili za kufanya mazoezi mkoani Morogoro ili wachezaji wazoee mazingira kabla ya kuivaa Mtibwa Sugar Jumapili
ADVERTISE HERE