Msimu huu Yanga imepania kufanya vizuri katika michuano yote ambayo timu zake zitashiriki
Usajili kabambe umefanyika kuboresha timu ya Wanaume na ile ya kina dada Yanga Princes itakayowania ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake, Serengeti Lite
Uongozi wa Yanga pia umekiimarisha kikosi cha timu ya vijana U20 ambacho baadae msimu huu kitashiriki ligi ya vijana
Kwa misimu ya karibuni Yanga B imetoa wachezaji wazuri ambao wameingia moja kwa moja kwenye timu ya wakubwa huku wengine wakijiunga na timu nyingine
Katika kikosi cha msimu huu, yupo mshambuliaji Adam Kiondo ambaye amepandishwa kutoka timu hiyo ya vijana
Lakini pia nyota kama Maka Edward (Morocco), Yusufu Mhilu (Kagera Sugar), Paulo Godfrey, Erick Msagati(Polisi Tanzania) wote ni zao la timu hiyo ya vijana
Vijana wa Yanga U20 wameanza mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Sheria kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali