Krmpotic ataka mabao mengi Morogoro

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Sep 2020
Krmpotic ataka mabao mengi Morogoro

Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic anaongoza maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki

Mserbia huyo msimu huu ameiongoza Yanga kupata ushindi katika michezo miwili na mmoja kutoka sare na kujikusanyia alama saba

Miongoni mwa maboresho ambayo aliahidi kufanya baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, ni katika safu ya ushambuliaji

Yanga imefunga bao moja tu kwenye kila mchezo iliyocheza, ni idadi ndogo ya mabao ukilinganisha na aina ya wachezaji walionao

Krmpotic amesema timu yake haina tatizo katika kutengeneza nafasi, changamoto iko kwenye matumizi ya nafas hizo kuzibadili kuwa mabao

"Sifurahishwi na idadi ya mabao ambao tumefunga, ni changamoto inayosababishwa na mambo mengi lakini muhimu tumeweka mkazo kuboresha eneo hili"

"Tutahakikisha washambuliaji wetu wanafunga mabao ya kutosha kutokana na nafasi ambazo zitapatikana kwa sababu kama tunaweza kushinda kwa kupata pointi tatu bila ya mabao mengi huenda ikawa shida kwetu huko mbele," alisema Krmpotic

Wafungaji wa mabao ya Yanga katika ligi mpaka sasa ni Michael Sarpong, Lamine Moro na Mukoko Tonombe

Sarpong atakuwa na nafasi ya kuongeza akaunti yake siku ya Jumapili pale uwanja wa Jamhuri wakati Yanga itakapokuwa mgeni wa Mtibwa Sugar

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’