Kwa mujibu wa takwimu, Yanga imeanza vyema msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita
Mpaka sasa ikiwa imecheza mechi tatu kwenye ligi, imeshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja hivyo kujikusanyia alama saba
Hizi ni alama tatu zaidi ya matokeo waliyokuwa wamepata msimu uliopita baada ya michezo mitatu
Lakini pia, mpaka sasa Yanga haijapoteza mchezo wowote ikiwa ni pamoja na mechi za kirafiki
Mabingwa hao wa kihistoria wameshinda mechi nne, wameruhusu bao moja tu katika michezo mitano waliyocheza (ligi na kirafiki) huku wakifunga mabao saba
Maeneo yanayoonekana kuimarika zaidi ni eneo la safu ya ulinzi, mabeki Yassin Mustafa, Kibwana Shomari, Lamine Moro na Bakari Nondo wakiwa na mwanzo mzuri
Bado wengi hawaridhishwi na idadi ya mabao yanayopatikana lakini yapo matumaini wakati utafika mabao yataongezeka
Wachezaji katika safu ya ushambuliaji wameonyesha kuwa na uwezo binafsi kinachokosekana ni muunganiko wa kitimu jambo ambalo litaondoka kadiri wanavyocheza pamoja
Matarajio ya wengi ni kuona Yanga inarudisha ule utamaduni wa kuwashushia wapinzani wake vifurushi vya mabao
Hili ni suala la muda tu hasa pale mifumo ya kocha Zlatko Krmpotic itakapokuwa 'imetiki'