Ule msako wa alama tatu Jumapili hii utakuwa mkoani Morogoro ambapo mabingwa wa kihistoria Yanga watashuka uwanja wa Jamhuri kuumana na Mtibwa Sugar Jumapili, Septemba 27
Wanayanga wa mkoani Morogoro na maeneo ya jirani wameaswa kujitokeza kwa wingi Jamhuri kuwapa hamasa wachezaji wao
Hii ndio kampeni ya msimu huu, alama tatu zinan'golewa popote, ni mwendo mdundo hadi ubingwa
Uongozi wa Yanga pamoja na wadhamini wametimiza wajibu kwa kuboresha timu, kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji na hata mazingira mazuri ya maandalizi
Sasa ni zamu ya mashabiki kuibeba timu yao. Hakuna ubishi, shabiki ni silaha muhimu kwa mafanikio ya timu yoyote
Achana na kampeni 'chafu' zinazoendeshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema Yanga, kikosi kiko imara na tukiongeza hamasa ya mashabiki, ushindi utapatikana popote
Unachotakiwa kufanya shabiki wa ukweli, jitokeze uwanja wa Jamhuri Jumapili, alama tatu zitapatikana pale