Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga David Molinga amesajiliwa na klabu ya Zesco United ya nchini Zambia
Molinga ametua kwa mabingwa hao wa zamani wa Zambia baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Yanga msimu huu
Mkataba wake na Yanga ulimalizika mwezi uliopita na uongozi wa Yanga kuamua kuachana nae
Aliitumikia Yanga kwa msimu mmoja, akifanikiw akufunga mabao 10 kwenye ligi na mabao mawili kwenye michuano ya kombe la FA
Zesco ilimaliza nafasi ya tano msimu uliomalizika ligi kuu ya Zambia, ikikosa nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha misimu nane
Zesco United pia imetangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake Mkuu George Lwandamina ambaye pia amewahi kuinoa klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE