Ni msako wa alama tatu kila mechi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2020
Ni msako wa alama tatu kila mechi

Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wake kuungana pamoja kuhakikisha timu inapata hamasa ya kutosha katika kila mchezo wa ligi watakaocheza

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa wiki, Jumapili ijayo Yanga inasafiri mkoani Morogoro kuifuata Mtibwa Sugar katika mchezo mwingine wa ugenini

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema lengo la Yanga msimu huu ni kutwaa ubingwa hivyo kila mchezo kwao ni fainali

Amesema wamejipanga kuhakikisha Yanga inashinda popote pale iwe nyumbani au ugenini

"Kama viongozi tunatimiza wajibu wetu, tunahakikisha wachezaji na benchi la ufundi wanakuwa na mazingira mazuri ya maandalizi hivyo tunawataka mashabiki wetu wahakikishe timu inapata hamasa ya kutosha kila mahali wanapocheza. Tunachohitaji ni kushinda kila mchezo unaokuja mbele yetu tuweze kuwa mabingwa"

"Kocha ametuhakikishia kuwa kikosi kinaekea kukaa sawa kwa sababu kilichokuwa kinasumbua ni kupata kikosi cha kwanza, baada ya mechi na Kagera, ametuambia kuna mabadiliko makubwa.

"Tunaamini katika muda uliobaki kabla ya kukutana na Mtibwa Sugar atakuwa ameboresha  zaidi na wachezaji wanaonekana wana morali nzuri kwa sababu mara nyingi tunakuwa nao kuwasapoti kambini," alisema Mwakalebela

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’