Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kimeanza maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Septemba 27 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Mabingwa hao wa kihistoria watakwenda Morogoro kuzisaka alama zote tatu katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Aidha kwa kocha Zlatko Krmpotic, ni nafasi ya kukiandaa kikosi chake kimbinu kuhakikisha wanapata matokeo katika mazingira ya uwanja mgumu wa Jamhuri
Dimba la Jamhuri ni miongoni mwa viwanja korofi ambavyo haviruhusu kupigwa kandanda la chinichini
Mipango ya Yanga ni kuhakikisha wanapata matokeo kila watakapoenda kucheza iwe nyumbani au ugenini
ADVERTISE HERE