Yanga yamalizana na Mkomola

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2017
Yanga yamalizana na Mkomola
Klabu ya Yanga imedhamiri kuunda upya kikosi chake kwa kusajili wachezaji vijana watakaoinufaisha klabu hiyo kwa miaka mingi.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kimesheheni wachezaji vijana wengi na kinaendelea na program ya kuwasajili wengine.

Taarifa za uhakika ni kwamba Yanga tayari imemalizana na mshambuliaji wa Serengeti Boys, Yohana Mkomola ambaye anatarajiwa kuanza kuitumikia Yanga kwenye mzunguuko wa pili ligi kuu ya Vodacom

Mkomola aling'ara na kikosi hicho ya timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za AFCON kwa vijana nchini Gabon mapema mwaka huu.

Mwezi Agosti 2017 alifuzu majaribio kwenye klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia lakini alishindwa kusajiliwa kwa kuwa umri wake ulikuwa chini ya miaka 18.

Etoile walimchukua kwenye Academy yao wakiwa na lengo la kumsajili wakati atakapotimiza umri.

Mkomola ataungana na wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga kutoka Serengeti Boyz, mlinda lango Ramadhani Kabwili na winga Said Mussa.

Baada ya kutwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo, msimu huu chini ya kocha George Lwandamina Yanga inasuka upya kikosi chake.

Mwishoni mwa msimu huenda ikaachana na wachezaji wengi ambao umri umewatupa mkono huku wale wa kigeni ambao wamekuwa majeruhi kwa muda mrefu wakiwa hatarini zaidi kuonyeshwa mlango wa kutokea
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’