Pamoja na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar leo, mashabiki wa Yanga wameonyesha kutoridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao katika mchezo huo
Timu imeonekana kucheza bila ya mpangilio, ubunifu ulikosekana kwenye eneo la kiungo na ushambuliaji
Mserbia Zlatko Krmpotic ana kazi ya kufanya kuhakikisha timu yake inapata muunganiko na kucheza kandanda safi ambalo ndio shauku ya mashabiki
Msimu huu Wanayanga hawana kingine wanachotaka zaidi ya ubingwa, hivyo hofu hii ya mashabiki iwe salamu kwa Krmpotic kuwa bado ana kazi ya kufanya
Yanga imesheheni wachezaji wenye ubora wa hali ya juu katika kila idara, hivyo ni matarajio ya wengi kushuhudia burudani katika kila mchezo ambao Yanga inashuka dimbani
Hamasa imekuwa kubwa msimu huu, ni kutokana na matarajio hasa baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye usajili
Bado naamini subira inahitajika kwani benchi la ufundi linastahili kupewa muda wa kuijenga timu. Wana takribani wiki tatu tu tangu waanze majukumu yao