Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kikosi cha tmu hiyo kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumamosi uwanja wa Kaitaba
Akizungumza baada ya mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa Kaitaba jioni ya leo, Mwakalebela amesema wamejipanga kushinda mchezo huo kesho
"Tumefanya maandalizi mazuri, jana tumefanya mazoezi hapa na leo tumekamilisha maandalizi ya mwisho, Vijana wako tayari, hatuna majeruhi wachezaji wote wana ari kusaka ushindi kesho"
"Kwenye mazoezi ya leo Mwalimu alipata muda wa kuandaa timu yake kimbinu zaidi. Tunashukuru tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wetu tangu siku ya jana tulipowasili. Tunatarajia watajitokeza kwa wingi siku ya kesho uwanjani kutuunga mkono," alisema Mwakalebela
Yanga imekamilisha maandalizi yake ya mwisho uwanja wa Kaitaba tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki




