Makali ya Mwamnyeto yawaibua Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2020
Makali ya Mwamnyeto yawaibua Coastal Union

Kiwango cha juu kinachoonyeshwa na beki kisiki wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto, kimemuibua Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mguto akitamba kuwa wameiuzia Yanga jembe la kazi

Mwamnyeto alitua Yanga dirisha la usajili lililopita akitoka klabu ya Coastal Union ikielezwa GSM wametoa kitita cha zaidi ya Tsh Milioni 120 kumnyakua kutoka kwa wagosi hao wa kaya

Ikumbukwe beki huyo pia alikuwa aliwaniwa na klabu ya Simba iliyozidiwa ujanja na Injinia Hersi Said ambaye alifanikisha usajili huo kibabe

Mguto amesema anaamini wadau wa soka nchini sasa wanaweza kuelewa kwa nini hawakuwa tayari kumuachia Mwamnyeto kwa dau la chini

"Watu walikuwa wanaona kama tunatania wakati tunasema huyu ndiye beki ghali zaidi nchini. Tulikiona kipaji chake, tunaendelea kumfuatilia na kumpa hamasa ili aweze kufanya vizuri zaidi"

"Mmeona alivyo na ubora wa kukabiliana na mpira ya juu sio rahisi mpira wa krosi upite juu yake. Ni mchezaji wenye utulivu wa hali ya juu hata kwa mipira ya chini"

"Tumewapatia Yanga beki mzuri, lakini pia wachezaji aliokutana nao pale Yanga nao ni wazuri. Nadhani Yanga msimu ujao kama watapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa watakuwa na timu imara sana," alisema Mguto

Mwamnyeto ametua na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga. Yeye na Lamine Moro wametengeneza pacha bora ya ulinzi ambayo wengi wanaitizama kuwa namba moja mpaka sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’