Kikosi cha Yanga usiku wa leo Jumatano (saa 1) kitashuka kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi kuumana na Mlendege Fc katika mchezo wa kujipima nguvu
Mchezo huu ni sehemu ya maandalizi ya mabingwa hao wa kihistoria kabla ya safari ya Bukoba kuifuata Kagera Sugar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu siku ya Jumamosi
Viingilio vya mchezo huo Mzunguko 5,000/- na VIP 10,000/-
Hii ni nafasi kwa kocha Zlatko Krmpotic kujaribu mbinu mpya alizowafundisha vijana wake
Bila shaka fundi Carlinhos leo atapewa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kuwapa burudani mashabiki wa watakaojitokeza kwa wingi pale Azam Complex
ADVERTISE HERE