Kikosi cha timu ya Yanga kesho Jumatano, saa 1 usiku kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege kutoka Visiwani Zanzibar katika uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba siku ya Jumamosi.
Msemaji wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema viingilio vya mchezo huo vitakuwa shilingi 5000 kwa mzunguko na VIP shilingi 10,000
Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic anaendelea kukisuka kikosi chake, anahitaji mechi za kirafiki ili kutengeneza kikosi cha ushindani

ADVERTISE HERE