Kwa sasa mlinda lango Metacha Mnata anatazamwa kama mlinda lango namba moja ndani ya kikosi cha Yanga pamoja na kuwa hatofautiani sana kwa ubora na wenzake Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili
Pamoja na ubora wake, ziko changamoto ambazo wengi wanadhani anapaswa kuzifanyia kazi ili awe bora zaidi
Zaidi ni katika utaratibu wa kuanzisha mashambulizi. Metacha hupendelea zaidi kupiga mpira mbele, utaratibu ambao makipa wengi wa kisasa hawautumii tena
Kwani kupiga mpira mbele bila ya malengo ni sawa na kuwarejeshea wapinzani mpira waje wakushambulie tena
Shikhalo huwa yuko vizuri sana kwenye kuanzisha mashambulizi, inapaswa mlinda lango awe mtu wa kwanza kuanza mashambulizi kutokea nyuma, huo ndio utaratibu wa kisasa
Katika mchezo dhidi Mbeya City mashabiki wengi hawakufurahishwa na utaratibu wa kubutua mpira mbele. Hata kocha Zlatko Krmpotic alilizungumza baada ya mchezo
"Tunakupongeza kwa kazi nzuri langoni, ila mambo yakubutua acha mipira yote unayobutua inafikia kwa maadui, tukikutana na timu bora ni hasara," maoni ya Mwanayanga Oliva Hadsone
"Hongera kwako lakini naomba ushauri wangu ufanyie kazi, wewe ni moja wa makipa wazuri sana Metach ila endapo utarekebisha ile tabia ya kubutua mipira mbele halafu kuna mtu mmoja mbele ni kuwapa wapinzani mali
"Mashambulizi anzia nyuma kwa mabeki wako na viungo na pia timu inapoongoza bao moja basi usifanye mzaha kwa kuchelewesha mda," Isai, mdau mwingine wa Yanga alitoa maoni yake