Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong ameeleza kuvutiwa na ushindani uliopo ligi kuu ya Vodacom
Sarpong alitua Yanga mwezi uliopita akitokea klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda
Mghana huyo amesema baada ya kucheza mechi mbili msimu huu, amebaini timu zote zimejipanga na anatarajia ushindani utakuwa hivyo kwa kila mchezo
Aidha, Sarpong amesema lengo lake ni kuhakikisha anaisaidia Yanga kufanya vizuri na kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi
"Ligi ya Tanzania ina ushindani mkubwa, kutokana na kila timu kujipanga kupata matokeo mazuri pindi inapokuwa uwanjani, ninaona jinsi timu zilivyojipanga vizuri kila moja inataka kushika nafasi ya juu," alisema Sarpong.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili 'jumba', amesema anafurahia maisha ndani ya kikosi cha Yanga kwani anapata sapoti kutoka kwa wachezaji, viongozi na hata mashabiki
"Ninashukuru nimepata ushirikiano kuanzia nilipofika sijaona tofauti yoyote, ninaahidi mashabiki wangu kufanya vizuri," alisema.
Sarpong tayari amefungua akaunti yake ya mabao msimu huu akifunga bao la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1