Mshambuliaji mpya wa Yanga Yacouba Songne ameeleza kufurahia kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Songne alijiunga na Yanga mwezi uliopita akitokea klabu ya Asante Kotoko ya Ghana
Tayari amehusika katika michezo yote miwili ya ligi, pamoja na kuwa ndio kwanza ana wiki mbili tangu atue Jangwani
"Nina furaha kubwa ya kuwa sehemu ya wachezaji wa timu hii (Yanga)," Songne aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii


Hili ni jambo jema kwa klabu ya Yanga pale mchezaji anapotamka kuwa na furaha
Songne ameonyesha kujitambua na kuthamini yale yanayofanywa na Yanga kuhakikisha ana mazingira mazuri yatakayomrahisishia kutimiza majukumu yake
ADVERTISE HERE