Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City jana, kikosi cha Yanga Jumamosi hii kitakuwa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kuumana na Kagera Sugar katika moja ya mechi za kukata na shoka
Yanga imejikusanyia alama nne kutoka mechi mbili walizocheza, wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya vijana hao wa Meckie Mexime
Kocha Zlatko Krmpotic ana siku tano za kuimarisha kikosi chake tayari kwa mchezo huo
Msimu uliopita Kagera Sugar ilikuwa moja ya timu zilizowapa wakati mgumu vijana wa Yanga wakati wakinolewa na kocha Luc Eymael
Hata hivyo chini Krmpotic tayari kuna mabadiliko yakiuchezaji yanaonekana yakichangiwa na ubora wa wachezaji
Ili uweze kuwa bingwa unapaswa kushinda mechi ngumu, hivyo Yanga haipaswi kuchagua wapi wanaondoka na alama tatu, iwe jijini Dar es salaam au mikoani, lengo ni moja tu, USHINDI