FT : Yanga 1-0 Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2020
FT : Yanga 1-0 Mbeya City

Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuichapa Mbeya City bao 1-0 katika mchezo mkali

Tofauti na ilivyokuwa ikitarajiwa, Mbeya City walikuja kushindana na Yanga, na hakika walitoa upinzani mkali

Shukrani kwa Carlinhos Carmo na Lamine Moro, mpira wa kona wa Carlinhos ulitua kichwani kwa Moro na kuiandikia Yanga bao hilo pekee kwenye dakika ya 87

Kocha wa Mbeya City Amri Said alitumia mfumo wa kujihami kwa muda mwingi huku akitumia mashambulizi ya kushitukiza

Yanga ilimiliki mpira kwa muda mwingi hasa kwenye kipindi cha pili lakini changamoto kubwa ilikuwa kuipenya safu ya ulinzi ya Mbeya City

Kuingia kwa Carlinhos kuliongeza faida kwa Yanga hasa kupitia mipira iliyokufa

Carlinhos amedhihirisha yeye ni fundi kwelikweli wa kutumia mguu wake wa kulia kwenye mipira ya adhabu

Ni mchezo ambao Yanga ilihitaji ushindi, muhimu, ushindi umepatikana

Hata hivyo bado kocha Zlatko Krmpotic ana kazi ya kutengeneza muunganiko wa kikosi chake hasa kwenye eneo la ushambuliaji

Timu imekuwa ikicheza vizuri kuanzia nyuma mpaka sehemu ya kiungo, eneo la ushambuliaji Mserbia huyo anahitaji kuboresha

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’