Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic anafahamu kikosi chake leo kinahitaji kupata ushindi mchezo dhidi ya Mbeya City
Ni baada ya kulazimishwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa kwanza msimu huu
Katika mchezo huo uliopigwa wiki iliyopita, Krmpotic alianza na kikosi cha wachezaji wazawa tisa, maproo wakiwa mlinda lango Farouk Shikhalo na mshambuliaji Michael Sarpong pekee
Mserbia huyo alieleza sababu ya kutowajumuisha baadhi ya nyota wengine wa kigeni ni kutokana na kuchelewa kwa ITC zao, hawakuwa sehemu ya mpango wa mchezo huo
Alitolea mfano wachezaji Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ITC zao ziliwasili saa mbili kabla ya mchezo akiwa tayari ameshaandaa timu yake kwa ajili ya kuwakabili Prisons
Lakini leo mambo yatakuwa tofauti, silaha zake zote muhimu zinatarajiwa kuwepo dimbani
Kisinda, Mukoko, Yacouba na Sarpong wote wanaweza kuanza leo
Hata Muangola Carlinhos leo mashabiki wa Yanga watarajie kumuona dimbani katika mchezo wake wa kwanza wa ligi
Wakati akiwa bado anaendelea kuimarika baada ya kukaa nyumbani kwa takribani miezi sita, tangu ligi ya Angola iliposimamiwa mwezi March, Krmpotic amedokeza kuwa fundi huyo wa mpira atakuwa na dakika zake katika mchezo wa leo
Mchezo huu ni kama fainali kwa Yanga, kwani matokeo tofauti na ushindi hayatakubalika