KMC na Dodoma Jijini zimeendeleza rekodi ya ushindi asilimia 100 msimu huu baada ya kushinda michezo yao leo
KMC imeichapa Prisons mabao 2-1 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya mabao baada ya kufikisha alama sita
Wakiwa kwenye msimu wao wa kwanza VPL, Dodoma Jiji wameshinda mchezo wao wa pili baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 2-0
Dodoma Jiji nayo imefikisha alama sita ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya KMC na Azam Fc
Mabingwa watetezi Simba wao wameponea chupuchupu kule mkoani Morogoro baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wakatamiwa wa Mtibwa Sugar

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili kwa mechi kadhaa kupigwa, Yanga ikitarajiwa kushuka katika uwanja wa Mkapa kuikabili Mbeya City
ADVERTISE HERE